Dr Chambo

Asante

Kwa Kanisa la Jimbo la Afrika

Neema na Amani kwenu katika Jina la Bwana wetu

Ni furaha iliyoje na fursa ya kipekee imekuwepo kutumika Kimamlaka kama Msimamizi mkuu wa kanisa letu katika jimbo la Afrika-Bara la uwenyeji wetu.

Read More

Kazi hii imekuwa ya maana sana kwa Samatha na mimi na tuna shukurani za dhati kuturuhusu kutembea nanyi, kuabudu nanyi, na kumtumikia Kristo kwa pamoja katika bara hili la kipekee.

Tumebarikiwa na maombi yenu, upendo wen una ukarimu wenu mwema. Kuanzia kwa makanisa ya mtaa, kwa mkusanyiko wa wilaya, taasisi za mafunzo na Nyanja za umisheni-uaminifu wenu kwa mwito wa Kiungu umetuvuvia na kututia moyo. Kanisa barani Afika liko hai na limejaa matumaini. Fauka ya changamoto nyingi, zinazowakabili, ushuhuda wenu unazidi kungโ€™ara Zaidi.

Samantha na mimi tumetajirishwa na muda wenu, tumejifunza kutoka kwa shuhuda zenu, tumeshiriki katika ibaada zenu, na kusherekea zri zenu za umisheni. Asanteni kutukaribisheni sio tu kama viongozi bali pia kama familia.

Afrika ni bara pana na changamano, lakini katika kila cona tuliotembelea tulitiwa moyo sana na uwepo wa Roho na uhai ulioko kwenye kanisa la Mnazareti. Nyinyi ni watu wa Imani iliyo kita mizizi, dhabiti na yenye furaha. Tunamshukuru Mungu kwa njia nyingi ambazo mnatumika, kutoa, kuomba, kufundisha na kuwafikia wengine kwa upendo wa Kristo.

Hivi karibuni dr Scott na Debbie Daniels wataanza kutumika kama Msimamizi mkuu-kimamlaka pamoja na mkewe. Nina ujasiri mtabarikiwa kwa uongozi wao, unyenyekevu na moyo wa kiuchungaji.

Ninapohitimisha hatamu yangu ya uongozi, tafadhali mjue Samantha pamoja nami tunazidi kuwabeba mioyoni mwetu, tunawapenda na kuwaombea.

Kwa shukurani nyingi na Furaha
Ndugu yenu katika Kristo
Fili Chambo
Shalom/Amani